SADAKA YA MOYO
Zaburi 51:16-17, isaya 57:15-19, yeremia
17:9-10, mwanzo 8:21, warumi 10:10, luka 6:43-45, mithali 23:15,26
Sadaka ni matoleo ya mwanadamu kwa Mungu, Kuthibitisha
utegemezi wa mambo yote kwa Mungu (mwanzo 4:3-7, mwanzo 8:20-21). Hivyo sadaka
ni kuonyesha hali ya kumilikiwa na unyoofu wa moyo mbele za Mungu (mwanzo
22:1-18). Kitu chochote huwa sadaka kama thamani yake inagharimu sehemu kubwa
ya uhai wa mtu (marko 12:41-44). Tena ni hiari ya mtu kutoa sadaka ama kuto
kutoa (kutoka 36:3). Katika mahusiano ya mtu na Mungu sadaka huwa ni kiashiria
kikubwa sana na ni ngumu kwa Mungu au mtu huyo kusahau kiashiria hicho maana
hutengeneza agano (zaburi 50:5).
Mwanadamu aliumbwa kuwa na ibada na katika
ibada hiyo ni hiari yake kutoa sadaka. Ibada hii ni maisha, katika maisha ya
mwanadamu ni kama safari ambayo kwa kutumia Imani ya Kristo Yesu tunafika
nyumbani kwa Mungu. Katika maisha kuna uhuru wa kuchagua moyo wako uambatane na
Mungu au Shetani. Kwa maana utachagua katika ibada yako utoe sadaka kwa Mungu
au kwa Shetani, ila ni vema sana kuulinda moyo kuliko kitu chochote maana ndipo
utokako uzima ( mithali 4:23 )
Hivyo mbali na mali au fedha kitu kilicho
na gharama sawa na uhai ni moyo wa mtu. Na ndio sadaka aliyo umbiwa kutoa kabla
ya kuingia katika uzima wa milele au mauti. Sio kwa kuukata moyo na kuuweka
madhabahuni bali kwa kuufanya moyo umwamini kristo kuwa Bwana na mwokozi na
kutii maagizo yake kama mtumwa wake. “Sadaka ya moyo ni toba” yaani moyo
waunyenyekevu kwa Mungu na uliopondeka (zaburi 51:17)
Maoni
Chapisha Maoni