UHURU WA MKRISTO
Mkristo ni mtu anaye
mwamini Mungu katika Roho na kweli, ni mtu anayeongozwa na Mungu (Roho wa
Mungu), ni mtu anayemwita Mungu Aba! Tenani ambaye Kristo anaishi ndani yake
ni mtu anayempenda Mungu.
Uhuru – ni hali ya kuijua
kweli na kuwa mbali na hali ya vifungo vya mapokeo au tamaduni, siasa, dhambi
ya awali ambayo si asili ya mwanadamu. Bali kuwa karibu na kweli ambayo ni enzi
ya Mungu (ufalme wa Mungu) iliyo asili ya mtu na iliyo kusudio la Mungu kabla
ya ulimwengu kuumbwa.
Ukweli humfanya mtu kuwa
huru- na ukweli ni habari njema tunayohubiriwa na Yesu kristo kama ilivyo
kwenye maandiko matakatifu (yohana 8:31-36)- lakini kweli ni Roho mtakatifu
atufundishaye mambo yote tangu kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu kwa shuhuda za
Kristo Yesu (yohana 16:13-14) Roho wa Mungu akikaa ndani yetu huo ndio uhuru
wetu
Lengo moja wapo la Yesu
kristo kuja duniani ni kumuweka mwanadamu kuwa huru (luka 4:18-21, isaya
61:1-9) hii ni sababu ya eye kuja na kusema maneno ya uhai, lakini pia
kuishinda dhambi na kupokonya funguo ya kuzimu na mauti ambayo ni nguvu ya
ufalme wa giza uliokuwa ukitawala na kuweka watu katika vifungo.
Mauti ilipata nguvu
kutokana na uasi wa adamu katika sheria ya Mungu (warumi 5:12-14) lakini kuja
kwa Yesu kristo ni kushinda dhambi kwa haki na kutawala kwa Imani na sio sheria
iletayo dhambi. Hivyo binadamu aokolewe si kwa matendo ya sharia bali kwa Imani
(). (warumi 6, mathayo 11:25-30)
Maoni
Chapisha Maoni