MAHUSIANO NA UPENDO BAINA YA MTU NA MUNGU
Kwa
maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila
mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele (Yohana 3:16). Ni hakika
kuwa Mungu aliupenda kwanza ulimwengu na ndivyo ilivyo siku zote kuwa Mungu
anatupenda sana na anashughulika na mambo yetu wakati wote.
Ili
tupasa na inatupasa tumpende kwa kushika amri zake na maneno yake lakini hilo
limekuwa mtihani kwa binadamu wengi. Hivyo kwa binadamu upendo ndio sheria kuu
na ya kwanza ili kuufikia ufalme wa Mungu (kumbukumbu 6:5) “mpende BWANA MUNGU
wako kwa moyo wako wote, kwa nguvu zako zote na kwa akili zako zote”.
Kama
ilivokuwa ‘imani’ kusikia na kutii neno la Kristo, na imani ikiwa timilifu
inajenga jumla ya utegemezi wa mambo yote kwa Kristo ambayo tuaiita ‘tumaini’. Basi
upendo nao huhakikiwa kutokana na Tumaini thabiti lakini haya mambo yote
Hufanywa na Roho wa Mungu kwa wanadamu, hayapo ndani ya uwezo wa Mwanadamu
mwenyewe (Warumi 5:4-5).
MAHUSIANO
Mtu
yeyote ampendaye Mungu hulishika neno
lake (Yohana 14:15). Hapo Mungu humpenda na ndipo mahusiano hujengwa, maana
Mungu huja na kuishi pamoja naye(Yohana 14:23). Tukumbuke kuwa Mungu ni Neno na
kila mtu ashikaye neno tayari anajenga mahusiano na Mungu (Yohana 1:1)
Ajabu
ni kwamba ni ngumu kulishika neno la Mungu bila kumwamini Kristo maana maandiko
yote matakatifu yanashuhudia juu yake na yanataka tumwamini yeye maana ndiye
anaye shughulika na mahusiano ya Mungu na Wanadamu kama Muunganishi. “Kila
amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele”. Bila Kristo hakuna mahusiano
baina ya Mungu na Mwanadamu.
Yohana
6
"37wote anipao Baba watakuja kwangu wala yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe…………………………………40kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye mwana na Kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; Nami nitamfufua siku ya Mwisho”.
UPENDO
Upendo hubeba mambo
mengi ikiwa ni pamoja na Imani, tumaini, rehema, neema, stala, ujasiri,
uvumilivu (1Petro 4:8, 1Wakoritho 13:4-8).
Kwa kifupi Mungu ni
upendo, mtu ayafanyae matendo yanayo thibitisha
upendo anamjua Mungu, maana upendo unatoka kwa Mungu(1 Yohana 4: 7-11). Tuseme basi upendo huthibitika kwa tendo
jema litokalo katika moyo wa mtu ambalo chanzo chake ni Mungu. Upendo sio
maneno matupu ya ulimi au jambo la kufurahisha au kunufaisha tu (Yohana
3:18-24) bali ni jambo litokalo kwa Mungu ambalo linampendeza Mungu.
Yesu
anampenda Mungu Baba (Yohana 14:31) lakini Mungu Baba anampenda sana Bwana
Yesu, mwana wake wa pekee (Yohana 15:9-13, Mathayo 3:17). Pia ulimwengu
unatakiwa kufahamu kuwa Mungu anapenda sana walimwengu hata akamtoa Mwana wake
wa peekee ili kila anaye mwamini asipotee bali awe na uzima wa milele.
Kuna
haja ya kujua mahusiano na upendo wa Mungu na wanadamu kwa undani hasa katika
Nyanja ya mtu mmoja mmoja.
Mfano
Petro na Yohana, au Yakobo na Esau. Biblia inaonesha wazi kuwa Yesu alimpenda
sana Yohana, kuliko hata wanafunzi wake wengine, lakini Petro alionesha
kumpenda sana Kristo Yesu kuliko wanafunzi wengine. Pia katika agano la kale
kwenye maandiko matakatifu inaonesha Mungu anampenda sana Yakobo kuliko Esau
Pia
ukitizama jinsi Nabii Daniel alipenda utauwa na kutafuta sana maandiko na neno
la Mungu juu ya taifa lake la Israel kutoka kwenye vitabu vya manabii wengine
na kwa kufunga pamoja na sala. Hili lilimfanya kushika neno la Mungu na hilo
neno likakaa ndani yake. Hii ilipelekea Mungu ampende Daniel na kujidhihirisha
kwake mara kwa mara (Daniel 9:21-23, Yohana 14-21)
Binadamu
akitenda jambo Mungu analomuamuru basi
hawi mtumishi bali huwa rafiki (Yohana12,14,15) na uhusiano huonekana wazi.
Yakobo
alipendwa na Mungu kuliko Esau kaka yake, ni kutokana na utiifu aliokuwa nao.
Katika ndugu hawa wawili yaliibuka mataifa makubwa mawili. Yakobo ndie baba wa
taifa la Israel, na Esau ndiye baba wa taifa la Edom. Isreal ni taifa
lilipendwa na Mungu tangu awali, katika maandiko matakatifu inaonesha ndio
taifa ambalo ukombozi wa ulimwengu ulitakiwa uanzie kabla ya kuenda kwenye mataifa
mengine.
Ingawa
wana wa Israel (Yakobo) walishindwa kutii neno la Mungu na kukiuka amri zake.
Hivyo Mungu alituma manabii na wajumbe wengi kuwaokoa lakini waliwaua nakuzidi
pindua sheria za Mungu ili kufuata njia zao wenyewe. Lakini Mungu aliipenda Israel
na bado anaipenda, hivyo aliamua kuwakomboa kwa mkono wake mwenyewe yaani Yesu
kristo kusudi arejeshe mahusiano kwa neema na kwa njia ya imani. Ili kwa
kumwamini Yesu Kristo Israel ikombolewe lakini bado Israel haikumpenda Mungu (1
Yohana 4:8-9, Luka 13:34)
Kwa
sababu wana wa Israel walimkataa Mwenyenzi Mungu pamoja na neema ya ukombozi
wake. Basi ukombozi uliwekwa kuwa neema kwa mataifa yote ili Israel aone wivu
kwa ajili ya utukufu wa Mungu(Warumi 10:19). Mungu aliamua kuukomboa ulimwengu
wote na hasa kwa wale waliokuwa tayari kumpokea na kumwamini Yesu Kristo. Hivyo
Mungu huwapenda wale wanaomwamini na kumtii tena huwaokoa kwa neema na rehema
nyingi na kuwafanya kuwa wana wake (Yohana 1:11-13, Efeso 2:8-9).
Binadamu
hawezi kuwa timilifu pasipo Kumpenda Mungu. Tukimpenda Mungu kwanza ndipo tunaweza
kusema tunawapenda binadamu wenzetu, kwamaana Mungu huja na kuishi pamoa nasi
na kujidhihirisha kwetu. Mungu anatupenda wanadamu wote ikiwa tukimpenda na
sisi kwa moyo wetu wote, kwa nguvu zetu zote, na kwa akili zetu zote basi
tutakuwa salama na kuurithi ufalme udumuo milele katika uzima wake (Efeso
2:17-19)
Maoni
Chapisha Maoni