TUMAINI KATIKA KRISTO YESU

TUMAINI KATIKA KRISTO YESU
Tumeifunza kuwa imani ya mtu huanzishwa na Yesu mwenyewe na hutimizwa au huwa timilifu kwa uwezo wake mwenyewe. Hivyo binadamu hawezi kuamini bila kusikia neno la kristo na hawezi kulitimiza hilo neno pasipo Yesu, ambaye humtuma Roho mtakatifu kuwasaidia wanaomkubali kulitimiza neno lake.
Imani ikiwa thabiti hujenga tumaini katika kristo Yesu. Hivyo tumaini maana yake ni jumla ya utegemezi wa mambo yote kwa Yesu.
Watu wote wanaowamini Yesu katika kweli yote huwa na tumaini la uzima hata katika mauti (yohana 5:24-25) na hivyo huwa na tumaini la uzima wa milele. Lakini pia wanaomwamini Kristo kwa tumaini lote huushinda uovu na kuzimu. Wao huhesabiwa haki katika ufalme Mungu na hivyo nguvu za giza hazina mamlaka juu yao (wamtumainio bwana ni kama mlima sayuni)(Ayubu 1:10)
Wapo wamwaminio Kristo lakini wanakutana na majaribu mazito kama magonjwa sugu, umaskini, dhiki nyingi (Ayubu 1:21-22). Haya majaribu hayamaanishi kuwa ni matokeo ya dhambi au imani haba au kukosa tumaini kwa Kristo, bali ni kipimo cha imani zao katika Kristo, au kumuepusha mkristo na uovu(kujivuna) ili utukufu wa Mungu udhihilike,(2 Wakorintho 12:7) pia ni kawaida ya ulimwengu kuwa na dhiki kama hizo, basi vema kuwa na tumaini na kuwa na moyo mkuu kwa yeye aliye ushinda ulimwengu (Yohana 16:33)
Pia majaribu haya pengine mkristo huyo huyaombea sana na kufunga na kufanya kila njia lakini hayaondoki (2 Wakorintho 12:8). Kwa vile ni majaribu basi wapo wanaofeli kwa kutafuta njia mbadala kusuruhisha matatizo yao, hii hudhihilisha kuwa imani yao chanzo chake si thabiti na hata tumaini lao kwa Kristo halipo (alie jenga juu ya mchanga na aliejenga juu ya mwamba)
Wanaosimama katika imani kwa nia ya kumtumaini Mungu Imani yao hukua ma kumea na Neema ya Mungu huzidi kuwafunika (Warumi 5:3-5, Warumi 8:35) (wamtumainio bwana ni kama mlima sayuni)
Tumaini huanza baada ya imani ya Mtu kuwa timilifu na iliyofanywa na Kristo mwenyewe. Japo tumaini pasipo upendo haliwezi kuwa thabiti(huwa batili). Upendo utokanao na Tumaini thabiti hutengenezeka kutokana na mahusiano ya Mtu na Mungu (Yohana 3:16, Warumi 8:35-39). Na tumaini la mwanadamu linapatikana katika Nguvu za Roho Mtakatifu(Warumi 15:13)


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UHURU WA MKRISTO

MAHUSIANO NA UPENDO BAINA YA MTU NA MUNGU

MMEPEWA BURE TOENI BURE