UJANA
Umuhimu wa ujana Ujana ni hatua kubwa ya maisha ambayo kwa maisha ya mwanadamu ndio hatua ndefu yenye mambo mengi, na katika hatua hii nguvu na hisia hutawala lakini pia changamoto za maisha huibuka kwa wengi (mithali 16:9). Hatua ya ujana ni umri wa mtu kufanya maamuzi hivyo hekima inastahili kutumika kuliko nguvu na hisia/hulka (mhubiri 10:10, mithali 9:10) hapa ujana unahusisha wa kike na wakiume na wito ni huu “kumcha Mungu” wakati wa ujana “kumcha Mungu ni mwanzo wa hekima” (mithal 2:6, mithali 9:10, mithali 5:1-12, mithali 31:30) Hekima ya Mungu isipotuongoza katika ujana ni ngumu katika uzee kuipata (mhubiri 4:13). Pia tukumbuke binadamu wote tunazaliwa na ujinga mioyoni mwetu hivyo katika ujana ni hatua pekee ya kuweza kuushinda ujinga (mithali 22:15). Hatua za maisha Hatua kubwa za maisha zipo katika maeneo makubwa matatu utoto, ujana na uzee. (i) Eneo la utoto ni hatua ya kwanza na kiukweli ujinga ndio hutawala moyo wa mtoto (mithali 22:15, mithali 23:13-14) ...