MAHUSIANO NA UPENDO BAINA YA MTU NA MUNGU
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele (Yohana 3:16). Ni hakika kuwa Mungu aliupenda kwanza ulimwengu na ndivyo ilivyo siku zote kuwa Mungu anatupenda sana na anashughulika na mambo yetu wakati wote. Ili tupasa na inatupasa tumpende kwa kushika amri zake na maneno yake lakini hilo limekuwa mtihani kwa binadamu wengi. Hivyo kwa binadamu upendo ndio sheria kuu na ya kwanza ili kuufikia ufalme wa Mungu (kumbukumbu 6:5) “mpende BWANA MUNGU wako kwa moyo wako wote, kwa nguvu zako zote na kwa akili zako zote”. Kama ilivokuwa ‘imani’ kusikia na kutii neno la Kristo, na imani ikiwa timilifu inajenga jumla ya utegemezi wa mambo yote kwa Kristo ambayo tuaiita ‘tumaini’. Basi upendo nao huhakikiwa kutokana na Tumaini thabiti lakini haya mambo yote Hufanywa na Roho wa Mungu kwa wanadamu, hayapo ndani ya uwezo wa Mwanadamu mwenyewe (Warumi 5:4-5). MAHUSIANO Mtu yeyote ampendaye Mungu ...