Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2019

UJANA

Picha
Umuhimu wa ujana Ujana ni hatua kubwa ya maisha ambayo kwa maisha ya mwanadamu ndio hatua ndefu yenye mambo mengi, na katika hatua hii nguvu na hisia hutawala lakini pia changamoto za maisha huibuka kwa wengi (mithali 16:9). Hatua ya ujana ni umri wa mtu kufanya maamuzi hivyo hekima inastahili kutumika kuliko nguvu na hisia/hulka (mhubiri 10:10, mithali 9:10) hapa ujana unahusisha wa kike na wakiume na wito ni huu “kumcha Mungu” wakati wa ujana “kumcha Mungu ni mwanzo wa hekima” (mithal 2:6, mithali 9:10, mithali 5:1-12, mithali 31:30) Hekima ya Mungu isipotuongoza katika ujana ni ngumu katika uzee kuipata (mhubiri 4:13). Pia tukumbuke binadamu wote tunazaliwa na ujinga mioyoni mwetu hivyo katika ujana ni hatua pekee ya kuweza kuushinda ujinga (mithali 22:15). Hatua za maisha Hatua kubwa za maisha zipo katika maeneo makubwa matatu utoto, ujana na uzee. (i) Eneo la utoto ni hatua ya kwanza na kiukweli ujinga ndio hutawala moyo wa mtoto (mithali 22:15, mithali 23:13-14) ...

MMEPEWA BURE TOENI BURE

Picha
Hili neno kwa wengi wakilisikia basi hujua kuwa ni mafundisho ya kutaka sadaka, maana ndivyo linavyotumika mara nyingi tunapokuwa makanisani. Mmepewa vyote bure na toeni bure ni tabia ya Mungu wetu yaani kuwapa wanadamu neema kwa kila jambo (mfano wokovu, rehema, baraka). Hakuna kati ya wanadamu anayestahili mambo hayo, tunapewa bure tu. Hivyo Mungu anatutaka na sisi tuwe kama yeye maana tumeumbwa kwa mfano wake na sura yake (mwanzo 1:26-27, zaburi 82). Wanadamu wengi tunaogopa kupoteza mali au vitu vya thamani kwa kuwapa watu wengine. Kwa wasiwasi kwamba kesho tutaishi kwa taabu, lakini wakati mwingine Mungu anatupa afya njema bure ili tuwahudumie wenye maradhi, anatupa mali nyingi ili tusaidie wahitaji (zaburi82:3-4). Mungu anatubariki bure kwa vyeo ili tusaidie wanaoonewa na kupokonywa haki zao (zaburi 82:3). Japo kwa jinsi ulimwengu ulivyo tufundisha tunasaidia watu ili waje kutusaidia baadae (hapo tunasaidia watu wa karibu/wanaojiweza/wenye nafasi nzuri ili nasisi wat...

UHURU WA MKRISTO

Picha
Mkristo ni mtu anaye mwamini Mungu katika Roho na kweli, ni mtu anayeongozwa na Mungu (Roho wa Mungu), ni mtu anayemwita Mungu Aba! Tenani ambaye Kristo anaishi ndani yake ni mtu anayempenda Mungu. Uhuru – ni hali ya kuijua kweli na kuwa mbali na hali ya vifungo vya mapokeo au tamaduni, siasa, dhambi ya awali ambayo si asili ya mwanadamu. Bali kuwa karibu na kweli ambayo ni enzi ya Mungu (ufalme wa Mungu) iliyo asili ya mtu na iliyo kusudio la Mungu kabla ya ulimwengu kuumbwa. Ukweli humfanya mtu kuwa huru- na ukweli ni habari njema tunayohubiriwa na Yesu kristo kama ilivyo kwenye maandiko matakatifu (yohana 8:31-36)- lakini kweli ni Roho mtakatifu atufundishaye mambo yote tangu kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu kwa shuhuda za Kristo Yesu (yohana 16:13-14) Roho wa Mungu akikaa ndani yetu huo ndio uhuru wetu Lengo moja wapo la Yesu kristo kuja duniani ni kumuweka mwanadamu kuwa huru (luka 4:18-21, isaya 61:1-9) hii ni sababu ya eye kuja na kusema maneno ya uhai, lakini pia kuish...