SADAKA YA MOYO
Zaburi 51:16-17, isaya 57:15-19, yeremia 17:9-10, mwanzo 8:21, warumi 10:10, luka 6:43-45, mithali 23:15,26 Sadaka ni matoleo ya mwanadamu kwa Mungu, Kuthibitisha utegemezi wa mambo yote kwa Mungu (mwanzo 4:3-7, mwanzo 8:20-21). Hivyo sadaka ni kuonyesha hali ya kumilikiwa na unyoofu wa moyo mbele za Mungu (mwanzo 22:1-18). Kitu chochote huwa sadaka kama thamani yake inagharimu sehemu kubwa ya uhai wa mtu (marko 12:41-44). Tena ni hiari ya mtu kutoa sadaka ama kuto kutoa (kutoka 36:3). Katika mahusiano ya mtu na Mungu sadaka huwa ni kiashiria kikubwa sana na ni ngumu kwa Mungu au mtu huyo kusahau kiashiria hicho maana hutengeneza agano (zaburi 50:5). Mwanadamu aliumbwa kuwa na ibada na katika ibada hiyo ni hiari yake kutoa sadaka. Ibada hii ni maisha, katika maisha ya mwanadamu ni kama safari ambayo kwa kutumia Imani ya Kristo Yesu tunafika nyumbani kwa Mungu. Katika maisha kuna uhuru wa kuchagua moyo wako uambatane na Mungu au Shetani. Kwa maana utachagua katika ibada yako utoe...