UJANA

Umuhimu wa ujana
Ujana ni hatua kubwa ya maisha ambayo kwa maisha ya mwanadamu ndio hatua ndefu yenye mambo mengi, na katika hatua hii nguvu na hisia hutawala lakini pia changamoto za maisha huibuka kwa wengi (mithali 16:9). Hatua ya ujana ni umri wa mtu kufanya maamuzi hivyo hekima inastahili kutumika kuliko nguvu na hisia/hulka (mhubiri 10:10, mithali 9:10) hapa ujana unahusisha wa kike na wakiume na wito ni huu “kumcha Mungu” wakati wa ujana “kumcha Mungu ni mwanzo wa hekima” (mithal 2:6, mithali 9:10, mithali 5:1-12, mithali 31:30)
Hekima ya Mungu isipotuongoza katika ujana ni ngumu katika uzee kuipata (mhubiri 4:13). Pia tukumbuke binadamu wote tunazaliwa na ujinga mioyoni mwetu hivyo katika ujana ni hatua pekee ya kuweza kuushinda ujinga (mithali 22:15).
Hatua za maisha
Hatua kubwa za maisha zipo katika maeneo makubwa matatu utoto, ujana na uzee.
(i) Eneo la utoto
ni hatua ya kwanza na kiukweli ujinga ndio hutawala moyo wa mtoto (mithali 22:15, mithali 23:13-14) hatari ya ujinga ukikomaa huwa uovu hivyo kiboko, adhabu, na mafundisho ya Yesu Kristo ni haki kwa mtoto (1yohana 2:28). Maana hekima kwa mtoto huwa ni furaha kwa mzazi (mithali 23:15-16)
Ujinga ni jumla ya mambo yote mtu anayofanya pasipo fahamu nzuri ya maadili kwenye jamii, mambo hayo hutokana na tamaa/hisia/hulka (matakwa ya mwili) (wagalatia 5:17,19-21, 1yohana 2:16, 1yohana 2).
(ii) Eneo la ujana
Ni hatua inayohitaji kumcha Mungu sana ili kupata hekima na neema yake kuliko kuendelea kufuata mambo ya ujinga (mhubiri 12:1, mithali 9:10). Yesu kristo Mwenyewe alikua kwa kimo na hekima huku akimpendeza Mungu na wanadamu toka utotoni (luka 2:40,52).
Moyo wa mwanadamu hufanyika sehemu ya ibada ya kipekee tena ni sadaka kwa Mungu; ajabu ni kwamba moyo huharibiwa sana na mawazo ya uovu ya kumwasi Muumba kwenye umri wa ujana (mwanzo 8:21, yeremia 17:9-10, mithali 20:5). Hii ndio sababu Yesu Kristo anasema nipe Moyo wako (mithali 23:26,) pia mpende BWANA Mungu wako kwa Moyo wako wote (kumbukumbu 6:5) kwa roho yako yote na kwa nguvu zako zote. Tena wenye hekima walisema ‘mtumaini BWANA kwa moyo wako wote wala usitegemee akili zako mwenyewe (mithali 3:5) mkiri yeye, naye atanyosha mapito yako’ (mithali 3:6)
Neno la Mungu linashauri sana kulinda moyo kuliko yote tuyalindayo maana ndiko zitokako chemchem za uzima (mithali 4:23). Kama Mtu umeshindwa kuulinda moyo wako ungependa nani asaidie kuulinda Yesu kristo au ibilisi (mithali 13:3), kama ni kristo jua unatakiwa uyahifadhi maneno yake ushike amri zake ili uishi (mithali 4:4, mithali 14:33) ndipo atakapo kuja na kuishi na wewe (yohana 14:23-24)
BWANA akiwa pamoja nawe, unakuwa mfano wa shujaa mwenye kutisha, kwa hiyo hao wanaokuonea watajikwaa wala hawatashinda; watatahayarika sana. Kwa sababu hawakutenda kwa akili, wataona aibu ya milele ambayo haitasahauliwa kamwe (Yeremia 20:11).
Katika ujana endapo moyo wako utatumainia akili au nguvu au mtu au vitu kama mali, vyote hivi vitavunja moyo wako maana ndiyo hatma yake. Hakuna mwanadamu anaeweza kusaidia moyo wa mtu ukivunjika wala hakuna anaeweza kustahimili (mithali 18:14). Na ndio kusudi Mungu alimtuma Mwanae Yesu Kristo ili aje duniani kuganga waliovunjika moyo, na kuwatangazia mateka uhuru wao (isaya 61:1).
Moyo ni kitu cha thamani kwa Mungu ndio sababu alimtuma Yesu Kristo aje ulimwenguni kurudisha kile kilichopotea, yaani moyo uliokengeuka. Kwa moyo tunampenda (kumbu 6:5), kwa moyo tunaamini (warumi 10:10), kwa moyo tunamtii (mithali 4:4), kwa moyo tunamtumaini (mithali 3:5)
(iii) Eneo la uzee


Hii ni hatua ya mwisho ya maisha, hapa kuna uzee mwema na uzee mbaya ila katika uzee ni wakati wa kumbukumbu za ujana. Mtu anaweza kupata majuto au furaha ikitegemeana na hatma anayoiendea au na jinsi alivyoishi ujanani.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UHURU WA MKRISTO

MAHUSIANO NA UPENDO BAINA YA MTU NA MUNGU

SADAKA YA MOYO