MMEPEWA BURE TOENI BURE

Hili neno kwa wengi wakilisikia basi hujua kuwa ni mafundisho ya kutaka sadaka, maana ndivyo linavyotumika mara nyingi tunapokuwa makanisani.

Mmepewa vyote bure na toeni bure ni tabia ya Mungu wetu yaani kuwapa wanadamu neema kwa kila jambo (mfano wokovu, rehema, baraka). Hakuna kati ya wanadamu anayestahili mambo hayo, tunapewa bure tu. Hivyo Mungu anatutaka na sisi tuwe kama yeye maana tumeumbwa kwa mfano wake na sura yake (mwanzo 1:26-27, zaburi 82).
Wanadamu wengi tunaogopa kupoteza mali au vitu vya thamani kwa kuwapa watu wengine. Kwa wasiwasi kwamba kesho tutaishi kwa taabu, lakini wakati mwingine Mungu anatupa afya njema bure ili tuwahudumie wenye maradhi, anatupa mali nyingi ili tusaidie wahitaji (zaburi82:3-4). Mungu anatubariki bure kwa vyeo ili tusaidie wanaoonewa na kupokonywa haki zao (zaburi 82:3).
Japo kwa jinsi ulimwengu ulivyo tufundisha tunasaidia watu ili waje kutusaidia baadae (hapo tunasaidia watu wa karibu/wanaojiweza/wenye nafasi nzuri ili nasisi watukumbuke na watusaidie kwa nafasi zao. Isipotokea tunayotarajia tunajikuta katika hali ya uadui, kuchukiana, vinyongo na wivu katika mioyo yetu. Hii inafanya Marafiki zetu wawe wanaojiweza kiuchumi/maarufu/au wenye mamlaka kubwa pengine wenye mavazi na afya nzuri (mithali 19:4,6,7)
Anaetoa vipawa ni Mungu hivyo kila kipawa tulicho pewa bure lazima kitolewe bure (mathayo 25:14-15, waefeso 4:7-). Pia ni vema kuheshimu kipawa cha mwingine na vipawa vyetu nikwa faida ya jirani zetu wote tunaotakiwa kuwapenda kama nafsi zetu (1wakorintho 12:4-11, 2wakoritho 8:1-15,). Mara nyingi ulimwenguni jirani zetu ni watu wetu wa karibu (mume au mke), wazazi, ndugu, watu wa dini/dhehebu tofauti na sisi, watu mashuhuri, maskini, rangi/kabila tofauti, wenye tabia njema na wenye tabia mbaya machoni petu. Wote tuwapende kama nafsi zetu.
Kwa wale ambao ni watumishi wa Mungu yaani wale walioteuliwa na kristo Yesu ili kumtumikia (waefeso 4:11). Tunatakiwa kujua katika kuurithi ufalme wa mbinguni lazima tufanye kazi zote alizotupa maana mwamuzi/hakimu wetu atakuwa ni Kristo mwenyewe. Yeye atatupa hesabu yote kama tunahaki ama hatuna haki ya kuurithi ufalme wake uliowekwa tayari tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Tusije tukasema Bwana kwa jina lako tulihubiri na tulitoa pepo lakini atasema siwajui ninyi na akawaita wale wenye haki nakusema “njooni mliobarikiwa na Baba yangu, Urithini ufalme mliowekewa tayari….. kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika; nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni mkanijia” (mathayo 25:34-36, mathayo 7:21-23).
Kwa kupewa bure maisha ambayo tunasema mazuri basi tunanafasi ya kutoa bure pia. Hasa kwa wale wenye mahitaji na matatizo au shida ambao hata kurudisha fadhira ni ngumu. Maana Mungu hutufanyia hivyo, akitupa vitu vyote kwa neema tu na hata kurudisha hatuwezi. Mungu anataaka tuwe kama Yeye. Ndio dini ya kweli hiyo.

Hivyo tunapopewa mali nyingi au vyeo vikubwa na kuvikumbatia ili visipotee na kuwa na hofu ya kuibiwa au kunyang’anywa matokeo yake ni presha, tension, stress pengine kuanza kuwa na Imani kwa waganga, wachawi na mambo kama hayo. Wengine hujikuta katika ibada za makaburi.  

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UHURU WA MKRISTO

MAHUSIANO NA UPENDO BAINA YA MTU NA MUNGU

SADAKA YA MOYO