NENO KATIKA MOYO NA KATIKA KINYWA
Moyo
Tulivyojifunza awali kuwa
moyo ni sadaka ya pekee naya muhimu kumkabidhi Mungu yaani toba (isaya 57:15,
zaburi 32:1-5). Hata hivyo kwa moyo mtu huamini, kwani Imani ya mtu huwa moyoni
mwake (warumi 10:10). Pia ni vema kujua kuwa uhusiano wa Mungu na mtu hujengwa
moyoni kupitia njia ya Imani kwa Yesu kristo (warumi 5:1-11). Siku zote Imani
ya mwanadamu kwa Yesu kristo hudhihilisha upendo wake kwa Mungu, hivyo Imani
humpendeza Mungu, na upendo huo wa kweli ndio sheria iliyo kuu naya kwanza
kufuata (yohana 6:29, kumbukumbu 6:5)
Neno
Katika Moyo
Tukumbuke kuwa Mungu ni
Roho nao wamwabuduo katika kweli humwabudu katika Roho na kweli. Tafsiri ya
neno roho na moyo katika maandiko ya biblia takatifu yanashabihiana. Na mahali
pengine huonyesha kama roho huwa ndani ya moyo wa mtu. Pia tukumbuke tunaposema
Roho maana yake ni neno la Mungu yaani injili ya kweli inayo ambatana moja kwa
moja na Roho mtakatifu ambae ni Mungu (yohana 1:1, yohana 6:63, 1 wathesalonike
2:8, yohana 5:38)
Kumbe basi moyo wa mtu
ukitawaliwa na neno la Mungu na kuithibitisha Imani ya kweli katika kristo Yesu
mtu huyo huwa na mahusiano makubwa na Mungu (yohana 14:23). Japo watu wengi
hudhani kusemasema kwamba wanampenda Mungu na wanaimani na Yesu, wakati mioyo
yao ikijua dhahili kuwa wayasemayo si kweli ila ni kuwalaghai watu na
kuwatapeli ili wakidhi matakwa yao tu, hii ni kujidanganya, wasijue kuwa wanamtumikia
ibilisi, na kujipalia makaa ya hukumu kichwani, maana Mungu huchunguza mioyo (mathayo
24: 24, zaburi 78:36-37, yeremia 17:10, ufunuo 2:23)
Mtu ambaye moyo wake
hautawaliwi na maneno ya Mungu basi mwovu humtawala kirahisi (matendo 8:18-24,
waefeso 2:1-4). Na mwovu hudhani kuwa vile amemtawala mtu basi ni rahisi
kutawala wengine, kitu ambacho hatoweza kukifanya kwa mtu anae mwamini Yesu
kristo katika Roho na kweli (mathayo 4:1-11, luka 10:18-20, mathayo 5:48,)
Moyo wa mtu hutawaliwa
kwa neno, na maneno mtu ayasemayo yanatoka katika moyo wake (Luka 6:45) Mungu
ni Neno (yohana 1:1) na neno la Mungu ni Roho (yohana 6:63) na tukilishika neno
la Mungu ndipo Roho wake huja na ndani ya mioyo yetu na kututawala na kuishi
nasi (yohana 14:23-24)
Neno
Katika Kinywa
Basi neno litokalo kinywani
mwako ni kiashiria kikubwa kuonesha kama moyo wako unatawaliwa na Mungu au na
ibilisi au pengine na hisia zako za mwili (ayubu 22:22) Na kama ukitaka
kuijaribu roho kwa mtu anayedai kuwa anamwamini Mungu ni kwa kupitia meneno ya
kinywa chake (mathayo 15:18) hivyo tusipende kuamini kila roho.
Unajisi na haki ya mtu
hutokana na maneno yake. Siku zote limtokalo mtu limeujaza moyo wake (mathayo
15:10-20). Basi kama kwa kukiri tu mtu hupata haki na kwa moyo mtu akiamini
hupata wokovu, hivyo neno likitoka katika moyo wenye Imani ya kweli ni jambo
jema litokanalo na neema ya Mungu (warumi 10, mithali 18:21)
Karama za Mungu kama
wokovu, uponyaji, ulinzi, ukombozi hata ufufuo zinapatikana kama moyo unaamini
Yesu katika kweli yote na kwa kinywa unakiri Imani yako kwa kristo (kama moyo
wako unatawaliwa na Mungu maneno yako yamekuwa roho)
Tena ni vema kukumbuka
katika tafakari hii kuwa kila neno litahukumiwa mbele za Mungu lakini pia kila
neno jema litahesabiwa haki (mathayo 12:33-37).
Maoni
Chapisha Maoni