KUOMBA NA KUSIKILIZA
KUOMBA
Wanadamu
tunalojukumu la kuomba tunapoishi duniani, maombi huwa ya namna nyingi kama
maombi ya toba, shukrani, maombi ya sifa au kutukuza wakfu au nadhiri, kuomba
msaada, kuomba Baraka au fadhili kama uponyaji, muujiza, kuomba
kukilimishwa/kipawa/karama za Roho, suala la kuomba ni ibada ya muhimu na ni jambo la kila mtu lakini linahitaji
kuzingatia mambo yafuatayo;
Ø Kusali rohoni (yohana
4:23-24)
Kuomba
kwa moyo(moyoni) kunasaidia kuomba wakati wote kujizoeza kuomba moyoni ni faida
kwa mkristo. Neno linasema ni vema kuomba kila wakati bila kukoma (1 wathesalonike
5:17). Japo inawezekana kuwa ni ngumu kama tumezoea kuomba kwa kupayuka-payuka
(mathayo 6:7) tukiamini kwamba Mungu atatukumbuka kwenye shida zetu. Sina maana
kuwa ni vibaya kuomba kwa sauti ila nataka kusema kuna wakati wa kuomba kwa
sauti maana huwezi kuomba kwa sauti kila wakati na neno linatuhitaji kuomba
kila wakati.Neno pia linasema tusijisumbue kwa jambo lolote isipokuwa kwa
kusali na kuomba lakini haja zetu na zijulikane ( luka 21:34-36)
Mungu
ameufanya moyo kuwa chumba cha siri kwa ajili ya makutanio baina Yake na
binadamu. Mtu anapokuwa anaomba moyoni hakuna mtu anayeweza kujua hata awe
mwandani wako(mathayo 6:6, luka 7:39, mithali 4:23, )
Ø Jua haki zako kabla ya
kuomba( Daniel 9:7 )
kabla
ya kuomba nivema kujua haki zako katika ufalme wa Mungu( mathayo 6:33, isaya
51:1-2 isaya 53 ) haki zetu zinapatikana kupitia Yesu kristo mwenyewe (yeremia
4:2, yohana 16:9-10 zaburi 89:14). Alikufa msalabani ili tupate haki zote za
msingi ili tuishi duniani tupate uponyaji, uhuru toka kwenye vifungo vya
ibilisi, mahusiano na Mungu baba na tupate Baraka zote, na rehema za Mungu kwa
kupitia damu yake iliyomwagika msalabani. Kwa kifupi kila tunachoomba kwa Mungu
tunapata kupitia jina, na damu ya Yesu kristo (yohana 14:13-14, isaya 61:1-11).
Mungu anajua haja zetu hata kabla hatuja muomba (mathayo 6:8)
Ø Tambua nyakati za kuomba
(zaburi 32:6)
Kwa mtu mtauwa anafahamu ni wakati gani wa
kuomba, kumbe kuomba si suala la kujisikia bali kabla ya kuomba kuna mambo ya
kuzingatia, mtu mtauwa anapaswa kumwomba Mungu pale anapopatikana (zaburi 32:6)
na ni kweli tunapo mtafuta Mungu anapatikana (isaya 55:6) pia ni ngumu kumpata
Mungu tunapokuwa hatusikilizi nakutii maneno yake ( yeremia 7: 24, isaya 58:9)
Ø
Tuombe
kwa kuongozwa na Roho wa Mungu
Binadamu wengi hatujui kuomba kwa maana
tunaongozwa na matakwa ya miili yetu hivyo hisia na hulka ndo hutuongoza kwenye
maombi na sio Roho wa Mungu na matakwa yake. Matakwa ya Roho wa Mungu Ndio hayo
hayo matakwa ya Mungu (warumi 8:5-6,26-27,34-39). Mungu ni Roho tunapo muonba
lazima tuongozwe na Roho wake na hakikisha Roho wa Mungu anapopatikana ndipo
unapo muomba.
KUSIKILIZA
Kuomba ni vema kwa
binadamu lakini kusikiliza ni muhimu Zaidi (mhubiri 5:1-6)
Basi tunapofika mbele za Mungu,
tunapojisogeza mahali patakatifu pake ili tumuombe inabidi tumsikilize kwanza
(waebrania 4:16). Kwa maana Mungu anayajua mahitaji yetu kabla hatujamuomba.
Kusikiliza ni bora Zaidi kuliko kuomba vitu tusivovijua (mathayo 20:22, warumi
18:26, mhubiri 5:1). Tena kuomba wakati unaemuomba anajua haja zako na
anashughulika na mambo yako, ni sawa na kutomtambua Mungu na kazi kubwa
alizofanya kwako. Tuwe wepesi wa kusikiliza maagizo na kutekeleza na hiyo ndiyo
Imani na hasa ndiyo pekee inayo mpendeza Mungu (mhubiri 5:1,6, waebrania 11:1)
Mungu anatuagiza tumsikilize Yesu maana kwa kufanya hivyo tutaweza kuimalisha
Imani zetu (mathayo 17:3,5, mithali 8:34-35). Kumsikiliza Mungu ni muhimu sana ilikujiepusha
kuomba vitu vingi na tusivyo vijua au kulaumu na kujihesabia haki mbele za
Mungu (luka 18:9-14)
Maoni
Chapisha Maoni