KUTAMBUA NJIA YA MAISHA TUNAYOPITIA
Isaya
48:17 ”BWANA, Mkombozi wako,mtakatifu wa Israel, asema hivi; Mimi ni BWANA,
Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo
kuifuata”
Wengi
tunaishi duniani pasipo kufahamu njia tunayotakiwa tupitie hii hutufanya hata
katika majaribu madogo tuanguke kwa kukata tamaa, kuvunjika moyo na hata
kuangamia. Haya yanatupata katika Nyanja
tofautitofauti za maisha kama ndoa, urafiki, kazi, familia, masomo, na hata
katika umiliki wa mali. Tukiwa hatutambui njia tuipitayo ni rahisi kuangukia
kwenye utumwa, na vifungo vya ibilisi mpaka mauti. Mithali 14:12 “Iko njia
ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti”.
Binadamu
tunamahangaiko mengi hasa katika kutafuta mafanikio, kujenga mahusiano, na hata
kutafuta nguvu katika jamii. Watu wengi wanamali nyingi, elimu kubwa,
wake/waume wazuri, marafiki wema tena maarufu lakini bado hawatembei katika
njia iwapasayo. ”Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri
jicho langu likikutazama” (Zaburi 32:8). Mungu pekee huwaonyesha watu wapi pa
kupita maana kila mmoja aliumbwa katika mpango wake na malengo yake na kwa njia
moja tu ya imani watu wanapata nafasi ya kusikia shauri na maelekezo ya Mungu
na hivyo kutii na kufuata makusudio ya Mungu. Hiyo ndiyo njia impasayo mtu
kuifuata.
Wengi
wanashindwa kuelewa wanaposoma Yohana 14:6 isemayo, “Yesu akamwambia, Mimi
ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi”. Huu
ni mstari muhimu sana kwa kila Binadamu
yaani, kale kabla ya kuja kwa Yesu watu walifikia Uzima na kwa Baba kwa kushika
torati (ila hata ivyo ni wachache sana wanaoweza kuitimiza sheria) lakini baada
ya Yesu kuja watu hufikia uzima na kwa Mungu kwa kumuamini Yesu mwenyewe ndiyo
maana anasema “Mimi ndimi njia” yaani tukimwamini Yeye katika kweli yake
tutafika kwenye Uzima wa Mungu
Zipo
njia zinazoonekana ngumu kwetu lakini ndio mpango wa Mungu na kuna njia rahisi
mno lakini tunakuwa tumepotea. Ajabu ni kwamba kuna wakati tunakuwa na mipango
mingi ambayo ni halali na mingine si halali ambayo nayo inatakiwa ithibitishwe
na Mungu Mwenyewe.
Mithali
16:1-4 imeeleza kwa mapana kwamba “maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali
jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA. Njia zote za mtu ni safi machoni pake
mwenyewe; Bali BWANA huzipima roho za watu. Mkabidhi BWANA kazi zako, Na mawazo
yako yatathibitika. BWANA amefanya kila
kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya. Mistari hii inatupa
hitimisho kuwa maisha bila Yesu hakuna tunapoenda zaidi ya kuishi ili tufe bila
kufika Uzima wa Milele. TUMUAMINI YESU YEYE NI NJIA.
Maoni
Chapisha Maoni