NENO KATIKA MOYO NA KATIKA KINYWA
Moyo Tulivyojifunza awali kuwa moyo ni sadaka ya pekee naya muhimu kumkabidhi Mungu yaani toba (isaya 57:15, zaburi 32:1-5). Hata hivyo kwa moyo mtu huamini, kwani Imani ya mtu huwa moyoni mwake (warumi 10:10). Pia ni vema kujua kuwa uhusiano wa Mungu na mtu hujengwa moyoni kupitia njia ya Imani kwa Yesu kristo (warumi 5:1-11). Siku zote Imani ya mwanadamu kwa Yesu kristo hudhihilisha upendo wake kwa Mungu, hivyo Imani humpendeza Mungu, na upendo huo wa kweli ndio sheria iliyo kuu naya kwanza kufuata (yohana 6:29, kumbukumbu 6:5) Neno Katika Moyo Tukumbuke kuwa Mungu ni Roho nao wamwabuduo katika kweli humwabudu katika Roho na kweli. Tafsiri ya neno roho na moyo katika maandiko ya biblia takatifu yanashabihiana. Na mahali pengine huonyesha kama roho huwa ndani ya moyo wa mtu. Pia tukumbuke tunaposema Roho maana yake ni neno la Mungu yaani injili ya kweli inayo ambatana moja kwa moja na Roho mtakatifu ambae ni Mungu (yohana 1:1, yohana 6:63, 1 wathesalonike 2:8, yohana 5:38) ...