Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2017

IMANI NI KUSIKIA NA KUTII

Maandiko matakatifu yanatufundisha kuwa imani ni njia pekee ya kufikia Ufalme wa Mungu. Pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu (Waebrania 11:6). Sio kwa matoleo ya sadaka au kuhudumu katika nyumba zetu za ibada ndio tunaweza kumpendeza Mungu, bali ni kwa imani. Tafsiri ya imani ni kusikia na kutii neno litokalo kwa Kristo. Hivyo ni jukumu la kila mwanadamu kuamwamini Yesu Kristo ili kuufikia Ufalme wa Mungu. Imani katika Yesu kristo inahusisha mambo makubwa mawili yaani usikivu na utiifu. Usikivu ni hatua ya kwanza na utiifu ni hatua ya pili katika imani ajabu ni kwamba haya Yote mawili hufanywa na Yesu kristo mwenyewe na sio kwa nguvu za binadamu. 1.    Usikivu- ni kusikia neno litokalo kwa Kristo; binadamu wote walio wateule wanauwezo wa kusikia sauti ya Mungu na pia wanauwezo wa kusikia sauti ya Yesu kristo (1Yohana 4:6). Basi imani chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo (Warumi 10:17). Maandiko matakatifu yanaonyesha awali wana wa israeli (Ya...