Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2017

KUTAMBUA NJIA YA MAISHA TUNAYOPITIA

Isaya 48:17 ”BWANA, Mkombozi wako,mtakatifu wa Israel, asema hivi; Mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata” Wengi tunaishi duniani pasipo kufahamu njia tunayotakiwa tupitie hii hutufanya hata katika majaribu madogo tuanguke kwa kukata tamaa, kuvunjika moyo na hata kuangamia. Haya yanatupata  katika Nyanja tofautitofauti za maisha kama ndoa, urafiki, kazi, familia, masomo, na hata katika umiliki wa mali. Tukiwa hatutambui njia tuipitayo ni rahisi kuangukia kwenye utumwa, na vifungo vya ibilisi mpaka mauti. Mithali 14:12 “Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti”. Binadamu tunamahangaiko mengi hasa katika kutafuta mafanikio, kujenga mahusiano, na hata kutafuta nguvu katika jamii. Watu wengi wanamali nyingi, elimu kubwa, wake/waume wazuri, marafiki wema tena maarufu lakini bado hawatembei katika njia iwapasayo. ”Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri jich...